Mwenyezi Mungu Amesema : “ Sema; “ Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni mzoga au damu inayomwagika  au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kile ambacho kwa kuhalifiwa amri ya Mwenyezi Mungu kimechinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliyelazimika kula  pasipo kupenda wala kuchupa mipaka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.” Aya ya 145, Suratul An-aam.
UHAKIKA WA KISAYANSI

         Imekuja elimu kudiriki baadhi ya mambo yaliyokatazwa na sheria ya Kiislamu iliyohifadhiwa na wafuasi wake karne kwa karne kabla ya kugunduliwa kwa darubini na kwa mpangilio huo huo : Mzoga ambao bakteria hukua ndani yake, damu ambayo bakteria hukua ndani yake kwa kasi kubwa zaidi, hasa ikiwa ni nyingi,  na mwisho nguruwe ambapo katika mwili wake hukusanyika  jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa.

Read more...