Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema, “  Yussuf! Ewe mkweli ! Tueleze hakika ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe saba dhaifu. Na mashuke saba mabichi na mengine yamekauka, ili nirejee kwa watu wapate kujua. Akasema: “ Mtalima miaka saba mfululizo kwa juhudi (yaani limeni miaka saba kwa juhudi, kwani itaingia njaa kubwa baada ya miaka saba). Na mtakavyovivuna, viacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mnavyokula (ili mnavyoviacha mule miaka ya njaa itakayokuja.) Kisha inakuja baadaye miaka saba ya shida itakayokula vile mlivyoipa (yaani watu watakula ile akiba mliyoiweka) isipokuwa kidogo mtakachohifadhi (kwa ajili ya kupandia). Kisha baada ya haya, utakuja mwaka huo watu watasaidiwa na (Mwenyezi Mungu); na katika huo watakamua (vya kukamua).”

UHAKIKA WA KISAYANSI:

         Ufahamu wa kuhifadhi nafaka katika mashuke, unazingatiwa kuwa ni mpango muhimu wa kuhifadhi uzalishaji katika mazingira magumu mno.

Read more...