Mwenyezi Mungu Amesema, “ Ni mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule Aliyezijaalia nyota mbinguni, na Akajaalia humo jua na mwezi unaong’ara.” Aya ya 61 ya Suratul Furqan.
UKWELI WA KISAYANSI:
Nishati ya jua (mtambo wa nyuklia wa dunia). Hupatikana nishati ya jua kutokana na kuungua kwa haidrojeni ambayo ndiyo sehemu yake kuu na huigeuza kuwa helium ndani yake kwani wingi, shinikizo na joto linalofikia digirii milioni 15, hayo yote hupelekea kutokea kwa maingiliano ya nyuklia na kuchanganyika kwa atom nne za haidrojeni kwa ajili ya kutoa atom moja ya helium na inakuwa tofauti ya densiti baina ya mada zenye kuingia katika maingiliano na matokeo ya maingiliano huenea nishati ya sumaku umeme na huenea juu ya jua mionzi yenye mawimbi madogo yanayoambatana na mionzi ya kuonekana, mionzi myekundu na mionzi ya zambarau. Hii ina maana ya kuwa jua linategemea nishati yake toka ndani yake kupitia kuchanganyika kwa kawaida kwa nyuklia katika hali kubwa ya shinikizo, density na joto, kama kwamba ni mtambo mkubwa wa nyuklia ili kuipatia ardhi mwangaza, ujoto na nishati. Jua ni nyota
Read more...