Mwenyezi Mungu Amesema, “ Ni mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule Aliyezijaalia nyota mbinguni, na Akajaalia humo jua na mwezi unaong’ara.” Aya ya 61 ya Suratul Furqan.

UKWELI WA KISAYANSI:

         Nishati ya jua (mtambo wa nyuklia wa dunia). Hupatikana nishati ya jua kutokana na kuungua kwa haidrojeni ambayo ndiyo sehemu yake kuu na huigeuza kuwa helium ndani yake kwani wingi, shinikizo na joto linalofikia digirii milioni 15, hayo yote hupelekea  kutokea kwa maingiliano ya nyuklia na kuchanganyika kwa atom nne za haidrojeni kwa ajili ya kutoa atom moja ya helium na inakuwa tofauti ya densiti baina ya mada zenye kuingia katika maingiliano na matokeo ya maingiliano huenea nishati ya sumaku umeme na huenea juu ya jua mionzi yenye mawimbi madogo yanayoambatana na mionzi ya kuonekana, mionzi myekundu na mionzi ya zambarau. Hii ina maana ya kuwa jua linategemea nishati yake toka ndani yake kupitia kuchanganyika kwa kawaida kwa nyuklia katika hali kubwa ya shinikizo, density na joto, kama kwamba ni mtambo mkubwa wa nyuklia ili kuipatia ardhi mwangaza, ujoto na nishati. Jua ni nyota  Mwenyezi Mungu Amesema, “ Ni mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule Aliyezijaalia nyota mbinguni, na Akajaalia humo jua na mwezi unaong’ara.” Aya ya 61 ya Suratul Furqan.

UKWELI WA KISAYANSI:

         Nishati ya jua (mtambo wa nyuklia wa dunia). Hupatikana nishati ya jua kutokana na kuungua kwa haidrojeni ambayo ndiyo sehemu yake kuu na huigeuza kuwa helium ndani yake kwani wingi, shinikizo na joto linalofikia digirii milioni 15, hayo yote hupelekea  kutokea kwa maingiliano ya nyuklia na kuchanganyika kwa atom nne za haidrojeni kwa ajili ya kutoa atom moja ya helium na inakuwa tofauti ya densiti baina ya mada zenye kuingia katika maingiliano na matokeo ya maingiliano huenea nishati ya sumaku umeme na huenea juu ya jua mionzi yenye mawimbi madogo yanayoambatana na mionzi ya kuonekana, mionzi myekundu na mionzi ya zambarau. Hii ina maana ya kuwa jua linategemea nishati yake toka ndani yake kupitia kuchanganyika kwa kawaida kwa nyuklia katika hali kubwa ya shinikizo, density na joto, kama kwamba ni mtambo mkubwa wa nyuklia ili kuipatia ardhi mwangaza, ujoto na nishati. Jua ni nyota, nayo ni kitu cha mbinguni kinachong’ara na kutoa nishati chenyewe wakati ambapo mwezi ni sayari, nayo ni kitu cha angani chenye mwangaza thabiti kinachotoa mionzi inayoipokea toka kwenye nyota na jua. Haya yanaambatana na matokeo ya kawaida ya sayari.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Maelezo ya Qurani tokea zaidi ya miaka elfu moja na mia nne, yameashiria tofauti baina ya nyota na sayari, mfano katika jua na mwezi. Nayo ndiyo yaliyofikiwa na wataalamu wa falaki wa leo baada ya kugundua darubini na kupiga picha za mwangaza  kwa nyota na sayari katika miaka michache iliyopita. Nyota si chengine isipokuwa ni kitu cha mbinguni chenye kung’ara kinachotoa nishati chenyewe wakati ambapo sayari ni kitu cha angani chenye mwangaza thabiti na kinachotoa mionzi inayokipokea toka  kwenye nyota na jua. Na haya yanaambatana na matokea ya kawaida ya sayari. Jua linahesabiwa kuwa ni mtambo mkubwa wa nyuklia unaoelea angani kwa kasi kubwa wenye mwangaza, nishati na joto yenye maumbo tofauti na yenye kubadilika katika idadi na namna. Nalo sio kisahani chenye kutoa mwangaza thabiti, bali ni taa yenye joto kali. (Na Tukaifanya taa ing’arayo na yenye joto kubwa). Suratul An Nabaa aya ya 13. Na mwezi ni sayari yenye kuakisi mwangaza wa jua na hutoa nuru kwa ardhi wakati wa usiku. Nalo ndilo ambalo limeelezewa na Qurani tukufu katika aya mbili hizi. Basi ni nani aliyemfahamisha Muhammad (S.A.W) ukweli huu? Hakika ni Mwenyezi Mungu iliyotukuka shani Yake