Mtume (S.A.W) amesema : “ Haukudhihiri uchafu katika kaumu katu hata wakautangaza, isipokuwa itaenea baina yao tauni na maradhi  ambayo hayakuwahi kutokea kwa waliotangulia ambao wamepita”

Pia Mtume (S.A.W) amesema : “ Haienei zina katika kaumu katu ila hukithiri vifo kwao.” Imepokelewa na Malik katika Muwatau.

UKWELI WA KISAYANSI:

         Sayansi ya kileo chini ya mikono ya wataalamu wa viumbe vidogo katika karne mbili zilizopita imegundua kuwa kundi la bacteria, ukungu na virusi, havimfikii binadamu isipokuwa kwa njia ya tendo la ngono la njia isiyo ya kawaida  Mtume (S.A.W) amesema : “ Haukudhihiri uchafu katika kaumu katu hata wakautangaza, isipokuwa itaenea baina yao tauni na maradhi  ambayo hayakuwahi kutokea kwa waliotangulia ambao wamepita”

Pia Mtume (S.A.W) amesema : “ Haienei zina katika kaumu katu ila hukithiri vifo kwao.” Imepokelewa na Malik katika Muwatau.

UKWELI WA KISAYANSI:

         Sayansi ya kileo chini ya mikono ya wataalamu wa viumbe vidogo katika karne mbili zilizopita imegundua kuwa kundi la bacteria, ukungu na virusi, havimfikii binadamu isipokuwa kwa njia ya tendo la ngono la njia isiyo ya kawaida. Ni kama kuwa na mahusiano mengi ya ngono yasiyo maalumu baina ya wanaume na wanawake, na mahusiano ya kimapenzi yasiyo ya kawaida baina ya wanaume kwa wanaume, au baina ya wanawake kwa wanawake . Na iwapo likitanuka duara la mahusiano hayo, basi jamii inatishiwa na magonjwa ya kuambukiza yasiyopata kutokea. Kwani vidudu hivyo vya maradhi hugeuka sifa zake bila ya kusita jambo ambalo yanayfanya kuwa sugu kutibika. Pia mwiliunashindwa kupambana navyo kwa sababu ya kutokuwepo kinga ya mwili dhidi yake. Na pia yanaweza kutokea kwa sura na sifa mpya katika mustakbali.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Hadithi ya Mtume (S.A.W) imetufichulia suna kuu ya kijamii inayoweza kutokea katika jamii yoyote inayofanyika na utangulizi na matokeo. Utangulizi: Kuenea mahusiano ya haramu kama zinaa na mahusiano yasiyo ya kawaida katika jamii na kutoyaharamisha na kuyaridhia, na kisha kuyatangazia. Nalo ndilo lililopewa jina la kuhalalisha ngono, nayo ndiyo yaliyomo kwenye kauli yake (S.A.W) “ Haukudhihiri uchafu katika kaumu katu hata wakautangazia). Matokeo yanayotokana na zinaa hiyo, ni kuenea kwa maradhi ya ngono na kutapakaa kwa sura ya kuambukiza kwa hatari, na kudhihiri kwake katika sura nyengine katika vizazi vinavyofuatia. Nayo ndiyo yaliyomo kwenye kauli yake (S.A.W) :  “Isipokuwa itaenea tauni na maradhi kwao ambayo hayakuwahi kutokea kwa waliowatangulia ambao wamepita”. Haya yametokea katika miaka hii katika jamii nyingi za Magharibi. Yameenea kwa mahusiano ya haramu na yasiyo ya kawaida, na wao wakayaridhia kama ni tabia ya kijamii, bali wameyatangazia kwa kila njia za matangazo zilizopo. Dk. Shofield katika kitabu chake cha  maradhi ya ngono anasema: Umeenea urahisi wa jamii kuelekea kwenye matendo yote ya ngono, na wala hakuna hisia yoyote ya haya kutokana na zinaa na kulawiti, au uhusiano wowote wa ngono usio wa kawaida au ulioharamishwa. Bali vyombo vya uenezi vimejaalia kuwa ni kitu cha aibu kwa mvulana na msichana kuwa ni mwenye kujikinga. Kujikinga kwa upande wa mwanamme au mwanamke katika jamii za magharibi, limekuwa ni jambo la kuonewa aibu na mtu. Vyombo vya habari vinatoa wito na kuhimiza zinaa kwa kuihesabu kuwa ni jambo la kimaumbile.

         Idara ya maelezo ya Uingereza inasema kuwa wenye mahusiano ya ngono yasiyo ya kawaida, wametoka kwenye duara lao la siri na kuingia kwenye duara la dhahiri, na wamekuwa na klabu zao, baa zao, mabustani yao, fukwe zao, mabwawa yao ya kuogelea na hata vyoo vyao.

         Yameandikwa mamia ya makala, vitabu, maigizo, hadithi na filamu zenye kutukuza umalaya na mahusiano ya ngono yasiyo ya kawaida, bali makanisa mengi ya Magharibi yameruhusu zinaa na kulawiti, bali hufungwa ndoa baina ya mwanamme na mwanamme mbele ya askofu katika baadhi ya makanisa ya Nchi za Magharibi. Yameundwa maelfu ya jumuiya na vilabu vinavyosimamia mambo ya wenye mahusiano ya ngono yasiyo ya kawaida. Umefikiwa utangulizi wa tabia hii inayoendelea. Je, yamefikiwa matokeo?

         Naam, yamedhihiri kwao maradhi ya zinaa katika sura ya maambukizo yaliyowasababishia machungu mengi. Ulimwengu umeshuhudia mawimbi makubwa ya kuenea kwa maradhi ya kaswende kwa vipindi tofauti tokea kudhihiri kwa mara ya kwanza mwaka 1494, na kufyeka mamilioni ya watu katika karne ya 15 iliyopita na kuharibu maisha ya mamilioni ya watu wengine. Bado vijidudu vya maradhi vinaendelea kubadilisha sifa zake na vinamshambulia upya binadamu katika ulimwengu wa leo. Kadhalika maradhi ya gono yanaongoza maradhi ya kuambukiza, nayo ni kati ya maradhi ya ngono yaliyoenea duniani na wenye kukata uzazi kwa mwenye kushambulia, kwa hiyo unaitwa ugamba mkubwa. Yote haya ni maradhi ya ngono yanayompata binadamu anayekwenda kinyume na mafunzo ya mbinguni  kwa magonjwa na maradhi yenye kuuma. Kisha hivi mwishoni, yamedhihiri maradhi ya ukimwi yanayotisha na yanayoua na ambayo virusi vyake huangamiza chombo cha kinga katika mwili wa binadamu. Kwa hiyo huangamiza viungo vyake kimoja baada ya chengine katika msururu wa maumivu ambayo hakuyajua binadamu hapo awali kabla ya kugunduliwa kwa virusi mwaka 1983. Kama hivi yametokea yaliyosemwa na Mtume (S.A.W). Hivyo hii sio dalili nyengine ya kuwa Muhammad (S.A.W) ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kweli?